KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, July 30, 2010

Kenya yawika mbio za mita 10,000

Mashindano ya 17 ya riadha barani afrika, yanaendelea katika uwanja wa Nyanyo mjini Nairobi.

Kenya ilianza mashindano hayo vyema kwa kutwaa medali ya dhahabu katika mbio za mita 10,000 kwa wanaume.

Wilson Kiprop, alihimili upinzani mkali kutoka kwa wanariadha wa Kenya, Uganda na mahasimu wa jadi Ethiopia, na kunyakuwa medali hiyo.

Uhasama uliotarajiwa kati ya wanariadha wa Kenya na Ethiopia haukujitokeza katika mbio hizo kwani Wakenya waliwika kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Moses Kipsiro akiridhika na medali ya fedha naye Mkenya Geofrey Mutahi akimaliza katika nafasi ya tatu kuchukua shaba.

Katika shindano la kurusha tufe kwa upande wa wanaume, Afrika Kusini ilinyakua medali zote tatu.


Wlison Kiprop
Burger Lambrechts alishinda dhahabu, Roelof Potgieter na Orazio Cremona walimaliza katika nafasi ya pili na tatu na kutwa medali fedha na shaba.

Katika fainali ya mchezo wa hammer, Amy Sene wa Senegal alishinda medali ya dhahabu naye Hussein Marwa wa Misri akinyakuwa medali ya fedha. Florence Edem Apefa wa Togo aliridhika na nafasi ya tatu na kushinda medali ya shaba.

Orodha ya medali

Kufikia sasa Afrika Kusini inaongoza kwenye msimamo wa medali na jumla ya medali tatu, moja ya dhahabu, fedha na shaba.

Kenya ni ya pili na medali mbili moja ya dhahabu na moja ya shaba. Senegal na Uganda zinashikilia nafasi ya tatu na medali moja ya fedha kila mmoja.
Nchi zingine ambazo zimejizolea medali ni pamoja na Misri na Togo.

Mpambano Alhamisi

Shindano kuu siku ya Alhamisi ni fainali ya mbio za mita 5000 kwa kina dada ambapo wanariadha 15 watamenyana.

Meseret Defar, wa Ethiopia anatarajiwa kutwa medali ya dhahabu. Defar ndiye mwanariadha ambaye ameandikisha muda bora zaidi katika mbio hizo mwaka huu wa muda wa dakika 14.46.25.

Wanariadha wengine wanaotarajiwa kuumpa defar ushindani mkali ni pamoja na Sentayehu Ejugu, Vivian Cheruiyot na Ines Chenonge wote wa Kenya.

Miongoni mwa mashindano mengine yatakayofanyika leo ni pamoja na raundi ya kwanza ya mbio za mita mia nane kwa kina dada ambako mshindi wa medali ya fedha katika mashindano ya Olimpiki Janeth Jepkosgei atapambana na wanariadha Makkhanya Mapaseka wa Afrika Kusini na Sahalima Hachlaf wa Morocco, ambao wameandikisha muda wa chini ya dakika mbili na sekundi nne mwaka huu.

Mbio nyingine ambazo zinatarajiwa kuwa na upinzani mkali ni mbio za mita mia nane, kwa wanaume ambapo Wakenya David Rudisha na Alfred Kirwa watamenya katika nusu fainali.

Mwanariadha wa Sudan amabye alitarajiwa na wengi kushinda medali Abubakar Kaki, alijiondoa.

No comments:

Post a Comment