KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, July 30, 2010

Wawili wafikishwa mahakaman kwa mauaji ya Prof. Mwaikusa


WATU wawili wakazi wa jijini Dar es Salaam, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana, wakikabiliwa na tuhuma za mauaji yaliyotokea ya aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria, Profesa Jwani Mwaikusa.
Waliofikishwa katika mahakama hiyo jana ni, Joseph Merema Machecho na mwenzake Jackson Zebedayo Chacha wote wakikabiliwa na mauaji ya profesa huyo.

Watuhumiwea hapo walifikishwa mbele ya Hakimu Gabriel Mirumb na kusomewa mashtaka na matatu yaliyoongozwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Anne Mwaipula.

Mwaipula alidai kuwa, washitakwia hao walitendakosa hilo la mauaji Julai 13, mwaka huu, nyumbani kwa profesa huyo maeneo la Salasala mtaa wa Mkonde, majira ya saa 3:40 usiku.

Washitakiwa walimuua Profesa Mwaikusa.
Pia washitakwioa hao waliweza kuua mwingine aliyetambulika kama Gwamaka Daudi na shtka la tatu pia kwa wakati huohuo walimuua mtu wa tatu ndani ya familia hiyo aliyetambulika John Mtui.

Kesi hiyo itatajwa tena Agosti 10, mwaka huu.

Mhadhiri huo aliuawa nyumbani kwake Julai 13, mwaka huu, baada watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kufika na silaha za moto na kumuua.

No comments:

Post a Comment