KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, July 30, 2010
Mtikila jela miezi sita
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala ya jijini Dar es Salaam, imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka sita jela Mchungaji Christopher Mtikila, baada kushindwa kulipa fedha anazodaiwa.
Hukumu hiyo ilitolewa jana ,mahakamani hapo na Hakimu Mfawidhi, Bi. Joyce Minde na kutakiwa kutumikia kifungo hicho ndani ya gereza la Ukonga.
Wakati hukumu hiyo ikitolewa Mtikila hakuwepo mahakamani na Hakimu kusema Mtikila ataanza kutumikia kifungo hicho mara tu mlalamikaji Bi, Paskazia Matete atakapowasilisha shilingi laki moja kwea ajili ya kumhudumia mdaiwa atakapokuwa gerezani.
Minde alimtaka mdai, kuwasilisha kila mwezi kiasi cha shilingi laki moja kwa ajili ya fedha ya kumkimu mdaiwa atakapokuwa gerezani.
"Mtikila ataanza kutumikia kifungo mara tu mdai atakapowasilisha fedha za kumhudumia katika matatizo mbalimbali likiwemo chakula," alisema Hakimu Minde
Hakimu Minde alisema kwa kuwa Mtikila muda mrefu hakulipa deni hilo na malalmikaji alitaka mdaiwa afungwe hivyo kutokana na kwa mujibu wa sheria mlalamikaji atawajibika kutoa kiasi hicho kwa ajili ya kumuhudumia Mtikila atakapokuwa gerezani na akitumikia kifungo hicho hatatakiwa kulipa deni analodaiwa.
Hakimu Minde alisema, kwa mujibu wa sheria mdaiwa hafungwi na alimtaka mlalamikaji kama endapo anafahamu mali za Mtikila anazozifahamu anaweza kuzikamata ziuzwe ili afidie fedha anayomdai na endapo angeweza kukamata na zikiuzwa na kufikia fedha anazomdai basi Mtikila hatotumikia kifungo hicho.
AWali Mtikila na mwenzake Mariam Issa, walidaiwa kumkopa malalamikaji Paskazia Matete kiasi cha shilingi milioni 9 na kisha wawili hao kushindwa kulipa deni hilo .
Mbali na hukumu hiyo Mtikila anakabiliwa na shataka lingine katika Mahakdama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kudaiwa kumkshifu Rais Kikwete kwa kumuita gaidi na kutoa maneno ya uchochezi.
Jana Mtikila aliwasili Mahakamani hapo na usafiri aina ya Bajaji kuwasilisha ombi la kutaka hakimu anayesikiliza shauri hilo afukuzwe kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment