KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, July 30, 2010

Ahukumiwa kunyongwa kwa kuua ablino

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mwanza, imemhukumu adhabu ya kifo baada ya kupatikana na kosa la mauaji ya mtoto aliyekuwa na ulemavu wa ngozi, Mariam Emmanueli (5).
Aliyehukumiwa kifungo hicho ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Kazimili Mashauri, huku mshitakiwa wa pili atika kesi hiyo aliachiwa huru na mahakamda hiyo.

Hukumu hiyo ilisomwa asubuhi jana, na Jaji Projest Rugazia baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka. .


Jaji alisema kautokana na ushahidi uliotolewa na shahidi wa pili uliridhisha wazi kwua mshitakwia huyo alihusika na kitendo hicho moja kwa moja kwa kuwa kabla ya siku ya tukio la mauaji, mshtakiwa huyo alimuuliza mshitakwia wa pili ni wapi mtoto huyo analala.

Na kuongeza siku ambayo mshitakwia huyo wa kwanza ali[pokwenda kukamatwa alionyesha dhahiri kuwa muoga kwa kuwa alijikojolea baada ya kuona askari wanakwenda kumkamata.


Hivyo kwa maelezo ya shahidi wa pili yaliyotolewa mahakamani hapo hayakuwa na shaka na alidai kuwa mara baada ya kuchinja marehemu huyo, mshitakiwa huyo alikinga damu kwa kutumia sufuria na ushahidi huo uliridhishwa kwa kuwa mama wa mtoto huyo alikiri kutoona damu alipoingia chumbani na ushahidi huo kudhihirisha wazi kuwa damu hiyo haikumwagika na ilikingwa kwa kutumia chombo hicho.


Mauaji hayo yalitokea Januari 21, mwaka 2008, majira ya saa 10 usiku katika kijiji cha Nyangh’olongo wilayani Misungwi, mkoani Mwanza.

No comments:

Post a Comment