Shirika la Umoja wa mataifa linaloshugulikia wakimbizi, limeitaka Saudi Arabia kuacha kuwarudisha nyumbani raia wa Somalia kwa lazima.
Shirika hilo la UNHCR, linasema watu 2,000 wamerejeshwa mjini Mogadishu hivi karibuni na sasa maisha yao yako hatarini.
Mapigano yamekuwa yakiendelea kila siku katika mji huo wa Mogadishu kati ya wanamgambo wa kiislamu, na majeshi ya serikali yanayoungwa mkono na majeshi ya Umoja wa Afrika.
Shirika la UNHCR, limetoa wito kwa nchi zote kutowarejesha raia wa Somalia katika maeneo ya Kusini na katikati mwa Somalia.
Baadhi ya maeneo hayo yako chini ya udhibiti wa wanamgambo wa al-Shabab, wanaohusishwa na kundi la kigaidi la al-Qaeda.
Wanamgambo wa Somalia
Wanamgambo wa Somalia
Serikali ya mpito ya Somalia, inadhibiti maeneo machache kati mji mkuu.
''Kutokana na hali machafuko mjini Mogadishu, shirika la UNHCR linatoa wito kwa viongozi wa Saudi kusitisha mipango yote ya kuwarejesha nyumbani raia wa Somalia,'' amesema msemaji wa shirika hilo Melissa Fleming.
Mzozo huo umesababisha raia wengi wa Somalia kukimbilia usalama katika nchi zingine, na baadhi hata huwalipa wasafirishaji haramu wa binadamu ambao huwasaidi kuvuka Ghuba ya Aden na kuingia nchini Yemen.
Baada ya kufika Yemen, kuna wale ambao huamua kuingia nchini Saudi Arabia.
Mji mkuu wa Somalia Mogadishu, na maeneo mengine ya Kusini mwa Somalia yamekuwa katika hali mzozo kwa takariban miongo miwili.
No comments:
Post a Comment