KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, July 31, 2010

Mugabe aomboleza kifo cha dada yake

Sabina Mugabe, mdogo wake wa kike Rais wa Zimbabwe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.

Alikuwa mbunge kwa miaka 23 mpaka mwaka 2008 alivyojiuzulu na alionekana kuwa mshirika wa karibu wa Robert Mugabe, mwenye umri wa miaka 86.

Chama cha Bw Mugabe cha Zanu-PF kimemtangaza kuwa shujaa wa kitaifa.

Hii inamaanisha atazikwa eneo la mashujaa, pahala pa heshima nje ya mji wa Harare ambapo wamezikwa waliopigana katika vita vya miaka ya 70 dhidi ya uongozi wa wazungu walio wachache.

Watoto wake wawili wa kiume nao pia waliwahi kuwa wabunge.

Mmoja ni Leo Mugabe, aliyekuwa mkuu wa chama cha mpira wa miguu cha Zimbabwe, na mwengine na Patrick Zhuwao, afisa mwandamizi wa Zanu-PF.

Amefariki dunia katika kliniki iliyopo kwenye mji mkuu wa Harare, baada ya kuumwa kwa muda mrefu.

Gazeti la serikali la Herald limeripoti kuwa Rais Mugabe aliwaambia waombolezaji kuwa dada yake alipata matatizo ya ubongo baada ya kupata kiharusi mwaka 1995.

Alisema, "Katika familia yetu, licha ya kuwa tumejaa huzuni, tunapata matumaini kwani marafiki zetu wote wako pamoja nasi."

Gazeti la Zimbabwe la Independent limeripoti kuwa chama cha Movement for Democratic Change, inayogawana madaraka na Zanu-PF, hakikushauriwa juu ya uamuzi wa kumpa Bi Mugabe hadhi ya ushujaa.

Alishutumiwa kwa kujinufaisha kutokana na utata wa mabadiliko ya mpango wa ardhi nchini humo na kuunga mkono uvamizi wa mashamba yaliyomilikiwa na wazungu.

No comments:

Post a Comment