KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, July 31, 2010

Wanne watozwa faini A Kusini kwa 'udhalilishaji'


Waafrika Kusini wazungu wanne wametozwa faini ya dola za kimarekani 2,700 kila mmoja kwa kutengeneza video ya kuwadhalilisha wafanyakazi watano weusi wa chuo kikuu na kuiweka kwenye wavuti.

Watu hao waliokuwa wanafunzi katika chuo kikuu cha Free State wamekubali mashtaka ya uhalifu wa kufanya madhara katika kesi hiyo iliyokuwepo siku ya Jumanne.

Video hiyo imewaonyesha wafanyakazi hao watano wakilazimishwa kupiga magoti na kulazimishwa kula chakula ambacho kilikojolewa na mmoja wa wanafunzi hao.

Video hiyo iliibua maandamano ya kupinga ubaguzi ilipotolewa hadharani mwaka 2008.

Kesi hiyo ilionekana muhimu sana katika nchi inayojaribu kuachana na ubaguzi uliokuwepo miaka iliyopita, miaka 16 tangu utawala wa wazungu umalizike.

Watu hao - - nao pia wamepewa kifungo cha miezi sita gerezani.

Faini za randi 20,000 ni zaidi ya kile kilichoombwa na waendesha mashtaka.

Hakimu Mziwonke Hinxa katika mji wa Bloemfontein wenye wazungu wengi zaidi alisema, " Hatua hii inatuma ujumbe mzito kwa wahalifu wa makosa kama haya."

Iwapo wanne hao hawatolipa faini hizo, watakabiliwa na miezi 12 jela.

Wafanyakazi hao watano wa chuo waliomba watu hao wanne watozwe faini, badala ya kufungwa gerezani.

Lakini wafanyakazi hao- wanaume wanne na mwanamke mmoja-wanatarajiwa kufungua kesi ya madai baada ya kesi hiyo ya uhalifu kuisha.

No comments:

Post a Comment