KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, July 31, 2010

Watatu watuhumiwa na shambulio la Uganda

akenya watatu wameshtakiwa kwa mauaji ya watu 76 waliouliwa wakati mabomu yalipolipuka walipokuwa wakitazama fainali ya Kombe la Dunia kupitia televisheni mjini Kampala, Uganda.

Hussein Hassan Agad, mwenye umri wa miaka 27, Mohamed Adan Abdow, 25 na Idris Magondu, 42, nao walishtakiwa kwa ugaidi na mashtaka 10 ya jaribio la mauaji.

Bado hawajajitetea na wataendelea kubaki kizuizini mpaka wafikishwe tena mahakamani Agosti 27.

Al-Shabab, kundi la wapiganaji la kisomali, lilisema lilihusika na mashambulio hayo.

Majeshi ya kutunza amani ya Uganda yapo Somalia, kusaidia serikali dhaifu, inayoungwa mkono na umoja wa mataifa dhidi ya al-Shabab, yenye uhusiano na al-Qaeda.

Umoja wa Afrika wiki hii iliahidi kuongeza majeshi ya kutunza amani Somalia kufikia majeshi 4,000, baada ya mkutano uliofanyika Kampala, mji uliokumbwa na mashambulio.

Mpaka sasa ni Uganda na Burundi tu ndizo zilizopeleka majeshi yake katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu na al-Shabab ilitishia kushambulia nchi zote mbili.
'Mhubiri wa Kiislamu'


Majeruhi wakipatiwa tiba wakati wa shambulio la Kampala

Milipuko ya Julai 11, ambayo pia iliwajeruhi watu 70, iliharibu kabisa klabu ya raga na mgahawa wa Kiethiopia wakati mashabiki wa soka walipokuwa wakitazama dakika za mwisho za fainali ya Kombe la Dunia.

Watu hao, wote wakiwa raia wa Kenya, walifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi siku ya Ijumaa mjini Kampala.

Karatasi ya mashtaka imemwelezea Hussein Hassan Agad kuwa "mhubiri wa kiislamu", huku Idris Magondu akiwa mfanyakazi wa kampuni moja mjini Nairobi, Kenya.

Watu hao walishtakiwa kwa makosa 89. Wanakabiliwa na makosa ya mauaji ya watu 61 kwa wale waliouliwa kwenye klabu ya raga ya Kyadondo na makosa 15 kwa wale waliouliwa kwenye mgahawa wa raia wa Ethiopia.

Mashtaka hayo pia yanajumuisha makosa matatu ya ugaidi na makosa 10 ya jaribio la mauaji.

Watu hao hawakuzungumza lolote walipofikishwa mahakamani.

Mwandishi wa BBC Ignatius Bahizi, aliyekuwa mahakamani, alisema watu hao walikamatwa Julai 12, siku moja baada ya mashambulio hayo.

Alisema, kulikuwa hamna ishara yeyote ya muda gani walikuwepo Uganda kabla ya mashambulio hayo.

Alisema takriban watu 27 walikamatwa na timu ya wachunguzi ya kimataifa, ikiwemo shirika la kijasusi la Marekani FBI.

Polisi wamesema watawafikisha washukiwa zaidi mahakamani katika siku za usoni

No comments:

Post a Comment