KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, July 23, 2010

Wachezaji wa soka wa Ufaransa waadhibiwa


Shirikisho la soka la Ufaransa, limewapiga marufuku wachezaji wote 23 wa kikosi cha timu ya taifa, kutocheza mechi ijayo.

Kocha mpya wa timu hiyo, Laurent Blanc, ameomba kuwa hangetaka kuona hata mchezaji mmoja wa timu iliyokuwepo akiitwa kushiriki mechi ya kirafiki dhidi ya Norway mjini Oslo, tarehe 11 Agosti.

Ufaransa kamwe haikupata ushindi katika mechi zake zote ilizoshiriki huko Afrika Kusini, na kocha mpya Laurent Blanc amesema hawezi kupuuza yaliyotokea huko Afrika kusini, chini ya kocha aliyeondoka, Raymond Domenech, na kusababisha kujiuzulu kwa rais wa shirikisho la mpira cha Ufaransa, Jean-Pierre Escalettes.

Wakati huohuo, shirikisho hilo limemkaribisha rais mpya, Fernand Duchaussoy.

Duchaussoy, mwenye umri wa miaka 67, amechaguliwa kama mkuu kwa muda, akitazamiwa kuimarisha tena soka ya Ufaransa, katika mwaka ambao udanganyifu, kashfa, wachezaji walioasi, na mchezo mbovu, ikiwa ni kati ya udhaifu uliojitokeza katika soka ya Ufaransa.

Alisema ni heshima kwake kukabidhiwa nafasi muhimu kama hiyo, lakini alielezea pia majuto kwamba anairithi kazi ya rafiki yake Jean-Pierre Escalettes, katika soka ya Ufaransa ikiwa katika hali mbaya mno, na mzozo wa kimichezo na vile vile kimaadili.

No comments:

Post a Comment