KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, July 23, 2010

Waathirika wa HIV wa miaka 50 waongezeka


Takwimu za hivi karibuni zimeonyesha kuwepo kwa ongezeko la watu wenye umri wa miaka 50 na zaidi wanaoambukizwa virusi vya ukimwi.

Maambukizi kwa watu wenye umri zaidi ya 50 huko England, Wales na Ireland ya kaskazini imeongezeka zaidi ya maradufu kwa kipindi cha chini ya muongo mmoja- kutoka maambukizi mapya 299 mwaka 2000 hadi 710 mwaka 2007.


Mtoto akipewa dawa za kufubaza ukimwi


Shirika la kulinda afya limesema mwaka 2008 kulikuwa na ubainishaji wa ugonjwa huo kwa watu 7,382 - asilimia nane miongoni mwao walikuwa zaidi ya umri wa miaka 50.

Wataalmu wanasema takwimu hizo ni kama ukumbusho wa umuhimu wa kufanya ngono salama, bila kujali umri.

Maambukizo mengine kwa njia ya kujamiiana nayo yameongezeka maradufu katika kipindi cha chini ya muongo mmoja na kwa watu wenye umri huo huo, huku ikiongezeka kuliko hata kwa vijana.

Ngono zembe
Ruth Smith, aliyeongoza utafiti wa HPA, alisema: " Tunakadiria karibu nusu ya watu wazima waliopimwa kati ya mwaka 2000 na 2007 wameambukizwa wakiwa na umri wa miaka 50 na zaidi. Hii inaonyesha umuhimu wa kupima virusi vya ukimwi- bila kujali umri.

" Lazima tuendelee kushawishi watu kufanya ngono iliyo salama- kutumia kondomu kwa wapenzi wa muda na wapya ni njia sahihi kuhakikisha watu hawaambukizwi na maradhi kwa njia ya kujamiiana kama vile ukimwi."

La kutia wasiwasi, watafiti hao wanasema, nusu ya watu hao walichelewa kupimwa. Virusi vya ukimwi vikitambulika mapema na mgonjwa kupata tiba, uwezekano wa kumwambukiza mwengine ni mdogo na mtu huweza kupata uwezo wa kuchagua tiba anayotaka.

Lisa Power, wa shirika la msaada la Terrrence Higgins, alisema uchunguzi wao uligundua watu wenye umri zaidi ya miaka 50 ni kundi lenye ongezeko la watu wenye virusi vya ukimwi Uingereza.

" Sababu mojawapo ni kwasababu watu wengi kwa sasa wanaishi na virusi hivyo kwa muda mrefu, tushukuru matibabu bora. Muda wa kuishi na virusi vya ukimwi umeongezeka."

Lakini amesema safari bado ni ndefu katika kusaidia kundi hilo.

Utafiti wote huu uliwakilishwa kwenye mkutano kuhusu ukimwi wa 2010 mjini Vienna.

No comments:

Post a Comment