KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, July 23, 2010

Brazil yapata kocha mpya, Muricy Ramalho


Timu ya taifa ya kandanda ya Brazil imempata kocha mpya Muricy Ramalho kushika nafasi ya Dunga aliyejiuzulu baada ya Brazil kutolewa mapema kwenye michuano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia nchini Afrika ya Kusini.

Ramalho ambaye ni kocha mkuu wa klabu ya Fluminense ya Rio de Janeiro, alijipatia umaarufu kwa kuiongoza klabu ya Sao Paulo kunyakua ubingwa wa Brazil kwa miaka mitatu mfululizo kati ya 2006 na 2008.

Ramalho anasifika kuwa ni miongoni mwa makocha hodari nchini Brazil na aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Brazil katika miaka ya 70.

Timu yake ya Fluminese hivi sasa ndiyo inaongoza ligi ya taifa ya Brazil na kuteuliwa kwake kumefurahiwa na wengi.

Je Ramalho atauweza mfupa aliouacha Dunga? Jibu litapatikana katika harakati za Brazil kujiandaa kwa Kombe la Dunia la 2014, fainali zitakazofanyika Brazil.

Ingawa, 2014 ni mbali sana kwa lugha ya soka, na kama matokeo ya awali yatakuwa mabovu kwake, basi ataonyeshwa mlango kama waliomtangulia.

No comments:

Post a Comment