KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, July 20, 2010

Ubunge, udiwani fomu kuanza kutolewa


CHAMA cha Mapinduzi leo kimeanza kutoa fomu za ugombea nafasi za ubunge na udiwani ambapo fomu hizo hutolewa kwa shilingi 100,000/
Akifafanua kuhusu fomu hizo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda , Richard Tambwe Hiza, alisema kwa wale wanaowania ubunge watachukua fomu hizo kwa shilingi 100,000 na udiwani zitatolewa kwa shilingi 10,000

Fomu hizo zitachukua ndani ya siku tatu na kuishia Julai 21 mwaka huu, na Kuanzia Julai 22 kampeni zitafunguliwa rasmi majimboni ambapo kila mmoja ataruhusiwa kujinadi na kumwaga sera zake kupitia chama hicho.

Hivyo leo shamra shamra zimetanda kwa wabunge wandaowania viti hivyo kwenda kuchukua fomu katika ofisi hizo.

No comments:

Post a Comment