KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, July 20, 2010

JK aenda Hispania


RAIS Jakaya Kikwete ameondoka nchini jana kwenda nchini Hispania kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa kujadili maendeleo ya Afrika ya kisiasa katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kikwete atahudhuria mkutano huo wa siku moja unaofanyika leo katika kituo cha mikutano ya kitaifa cha Palacio de Congresos de Madrid unaojulikana kama The African Progress Conference.

Lengo la mkutano huo unaokutanisha viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika ni kujadili maendeleo ya Afrika duniani.

Pia Rais Kikwete anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na mfalme wa Hispania Juan Carlos wa kwanza pamoja na Rais Zapatero wa nchi hiyo.

Washiriki wengine wa mkutano huo ni Ghana, Ivory Coast, Cape Verde, Kenya, Uingereza, Afrika Kusini, Mali, Ethiopia, Ureno, Msumbiji, Senegal, Ubelgiji, Equatorial Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)

No comments:

Post a Comment