KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, July 23, 2010
Trafigura yakutwa na makosa Ivory Coast
Mahakama ya Uholanzi imeikuta kampuni kubwa ya Trafigura ina makosa ya kusafirisha nje takataka zenye sumu kupitia bandari ya Amsterdam.
Mwaka 2006, Trafigura ilisafirisha takataka zinazodaiwa kuhusika na kuwajeruhi maelfu ya watu nchini Ivory Coast.
Trafigura ilikataa kuhusishwa na kosa lolote.
Kampuni hiyo pia imetozwa faini ya euro milioni moja kutokana na meli yake, Probo Koala, iliyopitia Amsterdam na mizigo yake kabla ya kuelekea Ivory Coast.
Hii ni mara ya kwanza kwa Trafigura kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu tangu kashfa ya takataka hizo za sumu kuibuliwa kwenye mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan, mwaka 2006.
Mwaka 2007 Trafigura iliilipa Ivory Coast dola za kimarekani milioni 160.
Trafigura pia ililipa dola za kimarekani milioni 50 katika kesi iliyomalizwa nje ya mahakama kwa raia wa Ivory Coast waliosema walioathirika na sumu hizo ziliposambazwa kwenye jaa maeneo mbalimbali Abidjan.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment