KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, July 22, 2010

Takukuru yatahadharisha wagombea


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewatahadhrisha wagombea ubunge kuachanda na vitendo vya kutoa rushwa kwa wananchi kwa lengo la kuchaguliwa.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dk. Edward Hoseah, wakati akiwatahadharisha wagombea hao kuhusiana na vitendo hivyo kwa kuwa tasisi hiyo itakuwa ikichunguza wagombea hao kuhusiana na vitendo hivyo.

Hayo yamekuja baada ya siku moja tu wagombea wa nafasi hizo kuanza kuchukua fomu kuwania nafasi hizo.

Mbali na kuwapa tahadhari wagombea hao pia aliwaasa Watanzania kwa ujumla kutokubali kupokea rushwa ya aina yoyote kutoka kwa wagombea hao kwa kuwa taasisi hiyo imeshasambaza vijana kila kona ya nchi kuwakamata watoa rushwa na wanaoshawishi vitendo hivyo ili sheria iweze kufata mkondo wake.

Amesema vijana hao wamesambazwa ili kuweza kuwafatilia wagombea hao kuhusina na suala zima la rushwa, na kutaka kila mtanzania awe mlinzi wa mwenzie katika vitendo hivyo.

"Ninawaomba sana Watanzania wasikubali kupokea chumvi, sabuni,vyakula au fedha ili iwe kigezo ya kumchagua mtu, sisi tumejipanga kila kona tunafuatilia, nimewaagiza makamanda wote wa mikoa waseme na waandishi wakikamata mtu au watu wanaotoa rushwa katika uchaguzi,"alisisitiza.

Tayari taaasisi hiyo imeshasambaza ujumbe maalum katiia simu za mkononi za kila mtumiaji wa simu hizo ili kuweza kuwa mmoja wa walinzi katika uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba mwaka huu.

"Atakayepewa rushwa tayari yeye atoe taarifa sehemu husika ili iwe kithibitisho cha rushwa hiyo" alisema

No comments:

Post a Comment