KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, July 22, 2010

Daladala yaingia mtoni


WATU idadi yao ambayo haikufahamika mara moja wamehofiwa kufa na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa baada ya basi la abiria kutumbukia kwenye Mto Kizinga uliopo Temeke.


Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 8 mchana, eneo hilo, ambako basi hilo la abiria aina ya Coaster, lenye namba za usajili T323 BEB, lilikuwa na abiria zaidi ya 30 ;lilikuwa likifanya safari zake kutokea Buguruni kwenda Mbagala Rangi tatu.

Ajali hiyo ilidaiwa kutokea baada ya kupasuka gurudumu la mbele la upande wa kushoto wakatilikiwa katika mwendo kasi.

Mara bada ya basi hilo kugonga kingo ya mto baadhi ya abiria walijinusuru kwa kutoka madirishani na wengine wakazidiwa baada yamlango wa basi hilo kugoma kufunguka.

Hivyo majeruhi waliwezwa kukimbizwa hospitalini kwa mtaibabu na wanne kati yao kukimbizwa Muhimbili kutokana na hali zao kuwa mbaya zaidi.

Majeruhiwa walioweza kutambulika ni Mariam Hassan, Omary Salum, Fikiri Awadh, Mwajuuma Hamis, Ismail Chonowa, Taabu Zuber, Salima Salehe, Said Jafari, Janeth James, Razaki Msangi, Pili Miraji, Shaban Msafiri, Sharifa Hamisi

No comments:

Post a Comment