KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, July 24, 2010

Slaa atashinda –Mbowe

KUFUATIa kuteuliwa kwa Mbunge wa Karatu, Dkt. Wilbrod Slaa awanie urais kwa tiketi ya chama hicho, chama hicho kimejinadi na kukiri uteuzi huo ni sahihi kwa kudai mgombea huyo atashinda urais mwaka huu.
Hayo yalielezwa na Mwenyekiti Tifa wa Chadema, Freeman Mbowe, alipokuwa akisoma maazimio yaliyofikiwa na Kamati Kuu ya chama hicho Chadema.

Mbowe alisema wameamua kumpendekeza Slaa kwa kuwa anakubalika na wananchi na kufaa katika kuwania kiti hicho.

Amesema Kamati Kuu ilizingatia umuhimu wa kumsimamisha mgombea makini na mwenye upeo na uwezo na mwenye uzalendo na uadilifu nchini.


Mbowe alisema nafasi hiyo ilifanyiwa utafiti na chama kwa muda mrefu na waliwashirikisha wadau kutokana na unyeti wake na hatimaye wakafikia maamuzi ya kukubaliana kumchagua Dk, Slaa.

"KWa kautokanfa na kumsimamisha Slaa, kuwania kitihicho mwaka huu, na kukubalika kwake kwenye ulingo wa siasa nchinini laime ashinde"Mbowe

Dkt. Slaa ni mmoja ya wabunge machachari nchini wanaopigania vikali kuteketeza ufisadi nchini na amejizosdlea sifa nyingi kuhusiana na upiganaji wakevita dhidi ya ufisadi.

No comments:

Post a Comment