KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, July 24, 2010

Ndugu wawili mbaroni kwa ubakaji

WANAFUNZI wawili vya vyuo vikuu ambao ndugu, wakazi wa Upanga jijini Dar es Salaam, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam wakikabiliwa na tuhuma za ubakaji kwa watoto wa kike wenye umri wa miaka 14 na 16.


Washitakiwa hao ni Elisha Ngenzi (24), ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Onesmo Ngenzi (26) mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Dar es Salaam (OUT)

Washitakwia hao wamepandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka kwa mahakimu tofauti ambapo Elisha alipandishwa mbele ya Hakimu Janeth Kinyage, na upande wa mashitaka ulikuwa ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka, Inspekta Msaidizi wa Polisi, Musa Gumbo.

Gumbo alidai kuwa, kosa hilo lilitendeka Julai 15, mwaka huu, katika mtaa wa Maliki eneo la Upanga, Dar es Salaam mshitakiwa alimuingilia binti wa miaka 16.

Gumbo alidai kuwa,mshitakiwa kabla ya kufanya tendo hilo alimuingiza vidole mtoto huyo sehemu zake za siri ili kuweza kufanikisha adhima yake hiyo na kudai kuwa binti huyo hakduwahi kuoingiliwa kimwili toka azaliwe.


Nae Onesmo alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Janeth Kaluyenda na upande wa mashitaka ulikuwa ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka Naima Mwanga.

Mwanga alidai kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo Julai 15, mwaka huu, katika eneo hilohilo na majira yanayofanana na kudai alimuingilia motto kimwili motto wa miaka 14 na kumnajisi.

Washitakiwa hao wote walirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyowataka kuwa na wadhamini wawili kila mmoja, watakaoweza kusaini hati ya Shilingi milioni mbili kila mmoja.

Kesi hiyo imeahirishwa naitarudi tena Agosti 5 mwaka huu, kwa kutajwa.

No comments:

Post a Comment