KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, July 27, 2010

Siko tayari kumkosa Asha

KIJANA aliyetambulika kwa jina moja la Othumani [31] mkazi wa Mikocheni amenusurika kifo baada ya kukutwa ameanza kunywa sumu aliyochanganya na soda
Kijana huyo alishaacha ujumbe usemao “ Siko tayari kumkosa Asha, sina umuhimu wakuishi” ulisema ujumbe huo

Mdogo wa wa Othumani aliingia chumbani na kumkuta ndugu yake huyo anakunywa soda na kushtuka na tukio hilo na kutoa taarifa kwa wengine na wakati wanafika hapo tayari sumu hiyo ambayo alishaanza kuitumia na macho kubadilika na kukimbizwa zahanati kwa huduma ya kwanza.

Ilidaiwa kijana huyo kulikuwa na mzozo wa kifamilia kati ya familia mbili hizo yake nay a mchumba wake.

Hivyo hadi habari hii inachapishwea kijana huyo bado yu ngali hospitali akipatiwa matibabu ya kuweza kurudisha afya yake irudi sawia.

Wakati huohuo, Lukas MBapila [75-80] mkazi wa Mwananyamala Msisiri jijini Dar es Salaam, amekutwa amejinyonga chumbani kwake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Bw. Elias Kalinga amesema mtu marehemu alikutwa ametumia kamba aina ya manila aliyoiunganisha na kanga kisha kuitundika katika dari la chumba chake.

Kalinga alisema saabasbu ya kufanya tendo hilo bado haijafahamika kwa kuwa marehemu hakuacha ujumbe wowote kuhusiana na adhamda yake hiyo.

Amesema upelelezi wakina unaendelea, mwili umehifadhiliwa katika hospitali ya Mwananyamala.

No comments:

Post a Comment