KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, July 27, 2010

kuweni makini -Chambo


WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam, wametakiwa kuwa makini na mafuta yanayouzwa mitaani kiholela baada ya baadhi ya wakazi kuuza mafuta ambayo hayafai kwa matumizi waliyoyazoa baada ya bomba la mafuta kupasuka baharini.
Hofu hiyo imekuja ni siku moja tu baada ya bomba la kusafirishia mafuta ya Kampuni ya TIPER lililoko Bandari ya Dar es Salaam kupasuka ma mafuta hayo kumwagika baharini.

Zaidi ya lita Milioni 10 za mafuta aina ya dizeli zilikwagika baharini na wananchid kukimbilia eneo la tukio kuzoa mafuta hayo kwa lengo la kujifanyia biashara.

Katibu Mkuu wa Wizara Miundombinu, Omar Chambo, alisema mafuta hayo hayafai kwa matumizi yoyote kutokana na kupoteza ubora baada ya kumwagiwa kemikali maalum ili kuyavunjavunja yasilete athari ndani ya bahari.

Bomba hilo lilipasuka wakati Mafuta hayo yakipitishwa chini ya bahari yakisukumwa kuelekea visima vya Oryx vilivyopo Kurasini.

No comments:

Post a Comment