KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, July 28, 2010

Mashujaa yaazimishwa kwa kuiombe nchi


KATIKA kuazimisha sikukuu ya kuwakumbuka mashujaa wa Tanzania, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja viongozid wa dini mbalimbali walikusanyika kuiombe nchi iwe katika hali ya amani na utulivu hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Mgeni rasmi katika maadhimisho, alikuwa Rais Jakaya Kikwete, ambapo alishiriki kuwakumbuka mshujaa hao pamoja aliweka mkuki na ngao katika mnara wa mashujaa kama ishara ya silaha za jadi zilizotumika wakati wa vita.

Dua hiyo upande wa kanisa Katoliki uliwakilishwa na Msinyori Julius Kangalawe, na upande wa dini uliwakilishwa na mjumbe kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Vilevile kulikuwa na mwakilishi kutoka Baraza la Wakristo Tanzania (CCT) ambao wote kwa pamoja waliiombea nchi kupata viongozi waadilifu na nchi kuendela na amani na utulivu.

Sikuuu hizo huazimishwa kila Julai 25, wa kila wmaka kuwakumbuka mashujaa waliopgana vita kuikomboa Tanzania ambayo hufanyika katika viwanja vya mnazi mmoja.

No comments:

Post a Comment