KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, July 18, 2010

Rufaa ya Liyumba Agosti 27

BAADA ya kutimiza takribani miezi miwili jela, Mahakama Kuu inatarajia kuanza kusikiliza rufaa wa aliyekuwa Mkurugenzi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba[62] Agosti 27, mwaka huu.

Mei 24, mwaka huu, Liyumba alihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kifungo cha kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la matumizi mabaya ya ofisi akiwa kazini.


Hivyo kutokana na hukumu wakili wake amekata rufaa kupinga hukumu hiyo na amepangiwa tarehe hiyo kuanza kusikilza rufaa hiyo ambayo wito wa kuitwa kwa Liyumba umeshamfikia katika Gereza la Ukonga anakotumika kifungo hicho.

Wakili mtetezi wa mshitakiwa, Majura Magafu alisema rafaa hiyo inatarajwia kusikili zwa na Jaji Emilian Mushi ka upande wa Jamuhuri.

No comments:

Post a Comment