KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, July 18, 2010

Atoweka nyumbani baada ya kujuzwa ukweli


MWANAFUNZI Rose [17] wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Uhuru Mchanganyiko ya Dar es Salaam, ametoweka nyumbani kwao kwa takribani wiki moja sasa kwa kile kinachohisiwa huenda ni kauli aliyotamkiwa na ndugu zake itakuwa imemuumiza kisaikolo
Mwanafunzi huyo mkazi wa Buguruni amekuwa haonekani nyumbani kwao hapo na kufanya walezi wa mwanafunzi huyo kuhaha huku na huko kumsaka mwanafunzi huyo bila mafanikio hadi kufikia jana.

Baada ya msichana huyo kutoonekana nyumbani hapo walianza kumsaka kwa ndugu na jamaa mbalimbali na bila mafanikio na juzi kutinga shuleni hapo kwa uongozi wa shule kuripoti tukio hilo ili wawezwe kusaidiwa.

Hata hivyo juhudi hizo pia hazikuzaa matunda baada ya kila rafiki wa binti huyo kudai hafahamu aliko rafiki yao huyo na kudai na wao hawajamuona toka shule ifunguliwe jumatatu ya wiki iliyopita.

Walipohojiwa kwa mara nyingine tena marafiki hao walijieleza na kila mmoja akidai kwa mara ya mwisho walionana kwenye masomo ya ziada [tuition] jumamosi ya wiki iliyopita na kuagana wataonana shule ikifunguliwa.

BAada ya majibu hayo mama huyo ambaye ni mlezi wa Rose, aliueleza uongozi wa shule hiyo kuwa, hawafahamu binti hyo atakuwa ameenda wapi na kusema kuna kosa limejitokeza nyumbani kwao hapo kwa Rose kutamkiwa maneno ambayo hakutegemea kuyasikia masikioni mwake na kuhisi labda kutokana tukio hilo

Mama huyo alidai kuwa” yeye ni mlezi wa Rose toka wazazi wake wafariki dunia na kuachiwa majukumu ya kumlea Rose toka yuko mtoto mdogo hajaanza shule ya msingi”

"Hivyo Rose toka anakua anajua mimi ndio mama yake mzazi wa kumzaa na mume wangu anafahamu ni baba yake mzazi wa kumzaa kwa miaka yote hiyo na hakufahamu ukweli kuhusu hilo, na wanangu mimi anajua ni ndugu zake wa kuzaliwa toka nitoke”

Alidai kulitokea mkwaruzano kati ya Rose na ndugu yake mmoja kutoka ndani ya familia hiyo na badala ya kugombana ndugu yake huyo alimtolea maneno na kumtobole ukwelu Rose kumwambia unaringa na wakati huna wazazi , na kumtobolewa ukweli wote kuhusu yeye

Sasa tokea hapo Rose baada ya kuambiwa hivyo na kubaini kuwa kumbe hao hawakuwa wazazi halali hakutaka maongezi zaidi na alipoaga kwenda shuleni hakurudi tena.

Baadae mama yake alipouliza ndio mtoto mmoja alipojaribu kumwambia ukweli kuwa dada yao alimwambia Rose maneno hayo mama huyo kubaki kilaumu kwa kitendo hicho na kulaumu aliyefanya kitendo hicho.

Habari hii itawajia zaidi

No comments:

Post a Comment