KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, July 18, 2010

Kinondoni yakithiri kwa uuzaji wa maeneo ya wazi



MANISPAA ya Kinondoni imebainika kuwa inaongoza kwa uuzaji wa maeneo ya wazi ikifuatiwa na Ilala na Temeke.
Hayo yalibainika jana baada ya kutolewa ripoti ya Kamati iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, kuchunguza uvamizi wa maeneo ya wazi jijini Dar es Salaam.

Kamati hiyo imebaini kuwa asilimia 80 ya maeneo ya wazi ndani ya Manispaa hiyo yamevamiwa isivyo halali na kubainika kuwa kulifanyika matumizi machafu ya ardhi isivyo halali.

Ripoti hiyo iliyosomwa na Mkurugenzi wa Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Albina Bura, alisema tume hiyo ilichunguza maeneo yapatayo 154 ya wazi ya Jiji na kati yao maeneo 110 ni ya Kinondoni.

Alisema kati ya hayo 110 yaliyochunguzwa Manispaa ya Kinondoni, 88 sawa na asilimia 80 yamebaniwa yamevamiwa.

Alisema katika Manispaa ya Ilala maeneo 30 ya wazi yalichunguzwa na kati yao, 11 sawa na asilimia 37 yamevamiwa wakati Temeke maeneo 14 yalichunguzwa na kati yao matano sawa na asilimia 14 yamevamiwa.


Katika sakata hilo la uuzwaji uliokithiri wa maeneo hayo, Mkuu wa Mkoa Dar es Salam, Willium Lukuvi aliwasimamisha kazi maofisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni na hatimaye alipandishwa kizimabani.

Wengine ni madiwani watano akiwamo Mstahiki Meya, Salum Londa na Naibu wake, Ibrahim Kisoki, aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Noel Mahyenga, nao walitiwa mbaroni.

No comments:

Post a Comment