KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, July 30, 2010

Housegirl auwa mtoto wa bosi, kisha na yeye kujinyonga

KATIKA hali isiyo yakawaida mfanyakazi wa kazi za ndani, aliyetambulika kwa jina moja la Zaina (16), amemuua mtoto wa bosi wake, Set Steven (2) kwa kumnyonga kisha naye kujinyonga.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana, maeneo ya Uwanja wa Ndege, mjini Morogoro.

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Bw. Thobias Andengenye, alisema kuwa, tukio hilo lilitokea majira ya saa 2:45 usiku, katika nyumba ya Steven Kapombe ambapo binti huyo alipokuwa akifanya kazi za ndani.

Alisema, Zaina alianza kumnyonga mtoto huyo kwa kutumia kipande cha kanga na baada ya kufanya mauaji hayo na yeye aliamua kujinyonga mwenyewe kwa kutumia kipande cha kanga pia alichokining'iniza juu ya dari.

Andengenye alisema, hadi sasa chanzo cha kufanya mauaji hayo bado hakijafahamika na polisi wanaendelea na uchunguzi kugundua chanzo cha vifo hivyo.

No comments:

Post a Comment