KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, July 1, 2010

Mapenzi Yanaua..


Afisa mmoja wa polisi nchini Malaysia amefariki dunia baada ya kuruka toka ghorofani ili kuzikwepa bakora za polisi wa kidini waliomfumania kwenye chumba cha hoteli akiwa na mwanamke ambaye si mke wake.
Katika tukio hilo lililotokea kwenye jimbo la Kelantan kaskazini mwa Malaysia, koplo wa polisi alifumaniwa kwenye chumba cha hoteli akiwa na mwanamke ambaye si mke wake.

"Afisa wa polisi mwenye umri wa miaka 33 alijaribu kuwatoroka polisi wa kidini waliovamia chumba chake kwa kupenya dirishani", ilisema taarifa ya polisi.

Taarifa hiyo ilisema kuwa inaaminika kuwa afisa huyo wa polisi aliruka toka kwenye dirisha lililopo ghorofa ya tatu.

"Alikuwa hai wakati alipokutwa chini kwenye kiwanja cha hoteli lakini alifariki baadae hospitalini", ilisema taarifa hiyo.

Polisi wa kidini walipoingia katika chumba alichokuwemo walimkuta mwanamke aliyekuwa naye na suruali moja ya kiume.

Mwanamke aliachiwa huru baada ya kuhojiwa na uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea.

Mkuu wa polisi wa Malaysia, Abdul Rahim Hanafi alilithibitishia shirika la habari la AFP kuwa afisa wake mmoja amefariki kwenye tukio hilo lakini alikataa kutoa maelezo zaidi.

Chini ya sheria za kiislamu zinazotumika kwa waislamu wa nchini Malaysia, ni marufuku kwa mwanaume na mwanamke ambao hawajaoana kuwa na ukaribu wa kimapenzi.

Polisi wa kidini huzitembelea hoteli na kumbi za starehe ili kuwanasa watu ambao hawajaoana wakikumbatiana au wakifanya mapenzi.

No comments:

Post a Comment