KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, July 3, 2010

Hodgson kocha mpya wa Liverpool

Klabu ya Liverpool imemtangaza Roy Hodgson kuwa meneja mpya wa klabu ya Liverpool baada ya kocha huyo wa zamani wa klabu ya Fulham kutia saini mkataba wa miaka 3.

Hodgson anachukua nafasi ya Rafael Benitez ambaye aliacha wadhifa huo kwa makubaliano na Liverpool, na sasa ni meneja wa klabu ya Intermilan.

Msimu uliopita Hodgson aliiongoza klabu ya Fulham hadi fainali ya Kombe la ligi ya Uropa, ambapo walipoteza kwa Atletico Madrid.

Katika muda wa miaka 34 ambayo Hodgson amehudumu kama meneja, Hodgson ameshazifundisha timu za taifa za Switzerland, Muungano wa Imarati na Finland.

Intermilan ni miongoni mwa vilabu 12 ambavyo Hodgson amevifundisha katika miaka hiyo.

Jukumu ambalo Mwingereza huyo atalipa umuhimu wa kwanza katika Liverpool ni kuhakikisha anawadumisha katika Anfield nahodha Steven Gerrard, mshambuliaji Fernando Torres na kiungo Javier Mascherano.
Rafael Benitez

Rafael Benitez

Kumekuwa na mazungumzo ya uwezekano wa wachezaji hao watatu kuondoka Liverpool kujiunga na vilabu vinavyoahidi pesa nono.

Ni wachezaji ambao Liverpool itawahitaji sana kufufua matumaini yao ya kurejea kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa wa Ulaya baada ya kukosa nafasi ya kushiriki msimu unaokuja, walipomaliza katika nafasi ya saba kwenye ligi ya primia ya England.

Mwenyekiti wa Liverpool Martin Broughton amemhakikishia Hodgson kwamba hatahitaji kuuza wachezaji ili kuweza kulipa deni kubwa la klabu hiyo linalofikia paundi milioni 350.

Hodgson alipigiwa kura ya kuwa meneja bora msimu uliopita baada ya kuiongoza Fulham hadi fainali ya kombe la Ligi ya Uropa, ambapo kabla ya hapo waliishinda Juventus ya Italia na Wolfsburg ya Ujerumani.Klabu ya Liverpool imemtangaza Roy Hodgson kuwa meneja mpya wa klabu ya Liverpool baada ya kocha huyo wa zamani wa klabu ya Fulham kutia saini mkataba wa miaka 3.

Hodgson anachukua nafasi ya Rafael Benitez ambaye aliacha wadhifa huo kwa makubaliano na Liverpool, na sasa ni meneja wa klabu ya Intermilan.

Msimu uliopita Hodgson aliiongoza klabu ya Fulham hadi fainali ya Kombe la ligi ya Uropa, ambapo walipoteza kwa Atletico Madrid.

Katika muda wa miaka 34 ambayo Hodgson amehudumu kama meneja, Hodgson ameshazifundisha timu za taifa za Switzerland, Muungano wa Imarati na Finland.

Intermilan ni miongoni mwa vilabu 12 ambavyo Hodgson amevifundisha katika miaka hiyo.

No comments:

Post a Comment