KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, July 1, 2010

Mtu Anapokilazimisha Kifo Chake..

Tukio hili la kusikitisha limetokea nchini Urusi ambapo mwanaume mmoja nchini humo alitumia nguvu zake zote kuwazuia watu wasimzuie kujirusha toka ghorofani, hatimaye alifariki baada ya kupigiza kichwa chake kwenye zege.
Picha ya tukio hilo la kusikitisha lililotokea mjini Moscow nchini Urusi, inamwonyesha mwanaume huyo akilazimisha kujirusha toka ghorofani ili afariki.

Jitihada za polisi na zimamoto kumshawishi asifanye hivyo zilishindwa kumshawishi mwanaume huyo kubadili uamuzi wake.

Nguvu ilitumika kuikamata miguu yake na kumvuta ndani lakini mateke aliyokuwa akirusha yaliwafanya zimamoto wazidiwe nguvu.

Muda si mrefu mwanaume huyo alifanikiwa kuchoropoka toka mikononi mwa zimamoto na kukipigiza kichwa chake kwenye zege. Alifariki hapo hapo kwenye eneo la tukio.

Sababu ya mwanaume huyo kuamua kujiua haijajulikana.

No comments:

Post a Comment