KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, July 27, 2010

Mafanikio katika maandalizi ya Olimpiki

Huku asilimia 70 ya ujenzi wa uwanja wa Olympic Park, ukiwa umemalizika waandalizi leo wanafanya maonyesho ya kusherehekea hatua zilizofikiwa.

Bingwa mara nne wa Olimpiki, Mmarekani Michael Johnson atakuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia ndani ya uwanja huo.

Naye mshindi wa mara nne wa medali ya dhahabu Muingereza Sir Chris Hoy,atafanya majaribio katika uwanja wa mashindano ya baiskeli.

Maafisa wanaoandaa mashindano ya Olimpiki, wanasema wameridhishwa na hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa uwanja huo na wamesema kwamba zimefikiwa mapema kuliko ilivyotarajiwa.

Hata hivyo kuna wasiwasi kuhusu gharama ya kuandaa mashindano hayo, ambayo itafikia pauni bilioni 9.28 hasa wakati huu ambapo kuna changamoto nyingi za kiuchumi.

Mapema mwaka huu, maandalizi hayo tayari yalikuwa yamegharimu pauni milioni 27.

Waandalizi sasa wanakabiliwa na tishio la bajeti yao kupunguzwa, wakati serikali itakapotangaza makadirio kamili ya matumizi ya fedha baadaye mwaka huu.

Kuna hofu kuwa huenda serikali ikaamua kupunguza fedha zilizowekwa kwa ajili ya mradi huo katika mpango wa kupunguza matumizi.

No comments:

Post a Comment