KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, July 27, 2010

AU kupeleka askari 2000 zaidi Somalia

Mkutano wa 15 wa viongozi wa nchi na serikali za Afrika unaotarajiwa kukamilika hii leo mjini Kampala, Uganda umeafikiana kuongeza majeshi zaidi nchini Somalia.

Maafisa wamesema kuwa AU imekubali kupeleka wanajeshi 2000 zaidi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Aidha, maafisa wa muungano huo wametangaza kuwa uwezo wa majeshi hayo huko Somalia utabadilika, ili kuwaruhusu wanajeshi kupambana na wanamgambo iwapo watabaini kushambuliwa.

Bado haijawa wazi wanajeshi watakaopelekwa Somalia watatoka nchi zipi. Hata hivyo awali, mwandishi wa BBC aliyeko Kampala, Uganda ambapo mkutano huo unafanyika, anasema awali nchi za Guinea na Djibouti zilitangaza kuwa zilikuwa tayari kutoa vikosi vya wanajeshi wao.

Awali, rais Museveni wa Uganda alitoa wito wa kuongezwa kwa jitihadi za kukabiliana na wapiganaji wa kundi la kiislamu la Al- Shabaab. Kundi hilo limekiri kufanya mashambulio ya Kampala, ambapo watu zaidi ya 76 walikufa, waliposhambuliwa wakitizama fainali za kombe la Dunia za 2010.

No comments:

Post a Comment