KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, July 30, 2010

Sitta akamatwa na Takukuru

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margaret Sitta, amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Tabora, akikabiliwa kutaka kugawa rushwa katika maandalizi ya uchaguzi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Naibu Kamanda wa Takukuru mkoani Tabora, Bruno Rwenyagira, ilisema kuwa Waziri Sitta alikamatwa juzi, majiara ya saa 7.45 mchana baada ya maofisa wa Taasisi hiyo kumfuatilia nyendo zake toka alipowasili mkoani humo.

Rwenyagira alisema kuwa, Sitta alikamatwa juzi akiwa na simu zipatazo saba aina ya NOKIA, bahasha 147 pamoja na fedha taslimu Shilingi. milioni moja na elfu kumi na tano 1,015,000.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa kutokana na Takukuru kumfatilia kwa kipindi kirefu toka alipowasili mkoani humo na kufatilia gari alilikuwa akilitumia aina ya Toyota Surf lenye namba za usajili T339ANL walibaini hayo na nWaziri huyo alipogundua hayo alihama hoteli aliyofikia na kuhama hapo.

Hata hivyo maofisa hao waliendelea kumfuatilia na kufanikiwa kumkamata majira ya saa 7.45 mchana juzi na taarifa hiyo kurushwa kwenye vyombo vya habari.

Waziri Sitta ni mke wa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, anawania uongozi ndani ya Umoja wa Wanawake Tanzania [UWT]

No comments:

Post a Comment