KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, July 23, 2010

Gazeti lamlipa Pitt na Jolie


Brad Pitt na Angelina Jolie wamekubali malipo ambayo hayakutangazwa kufuatia kesi ya madai ya kuingiliwa undani wa maisha yao na gazeti la News World.

Watu hao maarufu waliishtaki gazeti hilo mwezi Januari baada ya kuchapisha taarifa iliyosema kuwa watatengana.

Kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa katika mahakama kuu ya London, wakili wa wapenzi hao alisema magazeti hayo ya News Group sasa yamekubali kuwa madai hayo ni ya " uongo na yalikuwa yameingilia uhuru wao."

Wapenzi hao hawakuwepo wakati kesi hiyo ilipokuwa ikisikilizwa siku ya Alhamisi.

Taarifa hiyo ilidai kuwa Jolie na Pitt walimtembelea wakili anayeshughulika na masuala ya talaka Desemba 2009, na walifikia muafaka wa kugawana mali zao.

Lakini taarifa kutoka kwa mawakili wa Schillings iliarifu kuwa Sorrell Trope, ambaye amatambulishwa na baadhi ya magazeti kama ndiye alikuwa wakili wa kushughulikia masuala ya talaka, hakuwahi kuwaona wapenzi hao.

Katika mahakama hiyo Alhamis asubuhi, wakili Keith Schilling alisema News of the World, ambayo ilidai ilifanya hivyo kwa nia safi, imekubali kuchapisha msamaha kwenye gazeti lao.

Pia itamlipa Pitt na Jolie gharama zote, ambapo wana nia ya kuchangia kwenye shirika lao la kutoa msaada, wakfu wa Jolie-Pitt.

Gazeti hilo limethibitisha kuwepo na makubaliano, lakini limekataa kutoa maelezo zaidi.

No comments:

Post a Comment