KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, July 23, 2010

Burundi yaongoza kwa ulaji rushwa


Burundi imeipiku Kenya kwa kuwa nchi yenye rushwa zaidi katika Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa ya hivi karibuni ya shirika la Transparency International kuhusu suala la rushwa katika nchi za Afrika Mashariki, shirika hilo limetaja Mamlaka ya Kodi ya Burundi kuwa taasisi yenye kugubikwa zaidi na rushwa katika ukanda huu, ikifuatiwa na jeshi la polisi la nchi hiyo.

Jeshi la polisi la Kenya ambalo liliongoza kwa vitendo vya rushwa mwaka jana, katika ripoti ya sasa limeshika nafasi ya tatu.

Rwanda ndiyo nchi yenye matukio machache ya rushwa ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Shirika hilo liliwahoji watu elfu kumi mia tano katika nchi za Rwanda,Burundi, Kenya, Tanzania na Uganda kati ya mwezi wa Januari na Machi mwaka huu.

Waliohojiwa waliulizwa iwapo wamewahi kukumbana na wafanya kazi wa taasisi za umma ambao wamekuwa wakiomba rushwa ili kutoa huduma.

No comments:

Post a Comment