KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, July 8, 2010

Chatu Anapommeza Mamba..


Ilikuwa ni vita ya aina yake wakati wababe wawili chatu na mamba walipokutana kwenye bwawa moja mjini Florida nchini Marekani, katika vita hivyo chatu aliibuka mshindi kwa kumuua mamba lakini alipojaribu kummeza mamba mzima mzima, tumbo lake lilipasuka.
Katika tukio hilo ambalo ni nadra sana kutokea, mamba mwenye urefu wa mita mita 1.8 na chatu mwenye urefu wa mita 3.9 walikutana wakati kila mmoja akijitafutia chakula kwenye bwawa lililopo kwenye hifadhi ya wanyama ya Everglades ya mjini Florida.

Chatu baada ya kufanikiwa kumuua mamba alijaribu kummeza mamba huyo mzima mzima lakini tumbo lake lilipasuka baada ya kukamilisha nia yake hiyo.

Chatu huyo alikutwa akiwa amefariki huku mkia wa mamba ukiwa umechomoza kwenye sehemu ambao tumbo la chatu lilipasuka.

"Ni nadra sana kutokea kwa mapambano kama haya katika anga za wanyama pori", alisema Frank Mazzotti profesa wa wanyamapori wa chuo kikuu cha Florida.

"Inaonekana walikuwa na ukubwa sawa, yoyote anayekuwa wa mwanzo kumkamata mwenzake vizuri kabla ya mwenzake basi huwa mshindi" alisema Profesa Mazzotti.

Profesa Mazzotti alisema kuwa inawezekana mamba alilichoma kwa makucha yake tumbo la chatu na kupelekea lipasuke.

"Kwa kweli kama chatu ameweza kumuua mamba basi anaweza kukiua kiumbe chochote kile", aliongeza Profesa Mazzotti.

No comments:

Post a Comment