KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, July 19, 2010

Waafrika wadai vyakula bora - Ukimwi


Maelfu ya wataalamu wa afya wanakutana mjini Vienna kujadili suala la kukabliana na maradhi ya ukimwi.

Masuala yanayopewa kipaumbele kwenye mkutano huo ni pamoja na haki za watu walio katika uhusiano wa jinsia moja ambao wakati mwingine wanakabiliwa na changamoto ya kupata matibabu kwa kuwa wanabaguliwa.

Lakini barani Afrika wasiwasi mwingi upo katika utoaji wa vyakula muhimu vinavyohitajika kumudu afya ya walioambukizwa virusi hivyo.

Wengi wa walioambukizwa wanachagua kutotumia madawa hayo kwa kuwa yanamaliza nguvu kabisa mwilini ilhali wengi wao hawana fedha za kununua vyakula bora vitakavyorudisha nguvu haraka.

Evelyn Similoi, 31 kutoka Kenya, anasema kuwa hatumii madawa hayo na wala haugui kwa kuwa anakula vyakula bora kama njia mbadala ya kukabili makali ya ugonjwa huo.

Anasema kuwa licha ya kuwa madawa hayo yanapatikana kwa urahisi zaidi barani Afrika, suala la vyakula bora linahitaji kuangaziwa kwa makini zaidi.

No comments:

Post a Comment