KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, July 30, 2010

Aomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ana majini


MAHAMOUD SALUM (18), mkazi wa Tandika, amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kupatikana na kukiri kosa la kutishia kuua.
Hukumu hiyo ilitolewa jana, katika Mahakama ya Mwanzo Temeke,na Hakimu Mwinyiheri Kondo huku ikongozwa na Karani Blandina Haule, na hukumu hiyo kutolewa mara baada ya kukiri kosa hilo.

Mshitakiwa huyo alitakiwa kujitetea na Hakimu Kondo ili asimpe adhabu kali kwa kuwa aliirahisishia mahakama kukiri kosa hilo na ni moja ya taratibu za mahakama kabla ya kifungo mshitakwia anatakiwea ajitetee ili asipewe adhabu kali.

Mshitakiwa huyo alijitetea kama ifuatavyo ''Mheshimiwa hakimu naomba unipunguzie adhabu mbele ya Mahakama yako tukufu, naomba inipunguzie adhabu utakayonipa kwa kuwa mimi huwa ninasumbuliwa na majini, na mashetani muheshimiwa” hivyo gerezani yakinipata yaatanipa tabu kwa kuwa hawatajua wafanye nini” alijitetea mshitakiwa huyo.

Hata hivyo Hakimu hakuridhishwa na sababu hiyo na kuamua kumtwanga kifungo hicho ili iwe fundisho kutoa kauli za vitisho katika jamii na kunmuondolea uhuru mtu wa kuishi kwa sababu ambazo hazina msingi.

Awali hati ya mashitaka ilipofika mahakamani hapo, ilidaiwa kuwa, Julai 19, mwaka huu, majira ya saa 7 mchana, maeneo ya Mamboleo Tandika, mshitakiwa alimtishia mama yake mdogo aitwae Zeyanah Sultan kuwa lazima atammaliza kwa njuia yeyote ile yaani atamtoa uhai.

No comments:

Post a Comment