KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, June 2, 2010

Viongozi wa upinzani waonywa: Burundi


Serikali ya Burundi kupitia mawaziri wa ulinzi na usalama wa raia imetoa onyo kali kwa muungano wa vyama kumi na tatu vya upinzani vilivyopinga matokeo ya uchaguzi wa madiwani uliofanyika tarehe 24 mwezi uliopita wa Mei.

Serikali imetangaza kwamba vikosi vya usalama havitomvumilia yeyote yule anayekusudia kuzusha vurugu nchini Burundi.

Onyo hilo la serikali linafuatia habari kwamba vyama hivyo vina mpango wa kuhujumu usalama nchini Burundi.

Hapo jana wagombea urais watano walitangaza kutoshiriki katika uchaguzi huo wa urais wakidai kuwa chama tawala kinapanga kuiba kura.


Raia wa Burundi
Lakini chama chama tawala cha rais Pierre Nkurunziza kimepinga madai hayo na kusema, watano hao wanaogopa kushindwa.

Miongoni mwa viongozi hao waliojiondoa ni pamoja na aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi la National Liberation Forces, FNL, Agathon Rwasa ambaye angelikuwa mpinzani mkuu wa rais Nkurunziza.

Wiki iliyopita watano hao waliitisha kuvunjiliwa mbali ya tume ya uchaguzi baada ya uchaguzi wa udiwani uliokamilika tarehe 24 mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment