KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, June 2, 2010

Israel kuwaachilia wanaharakati

Serikali ya Israel imeanza kuwaachilia wanaharakati waliokamatwa kwenye meli zilizokuwa zinapeleka msaada Gaza na kisha kuwarejesha makwao.

Kwa mujibu wa Israel, meli hizo zilishambuliwa baada ya kukiuka marufuku iliyowekwa na Israel kuingiza bidhaa zozote katika Ukanda wa Gaza.

Zaidi ya wanaharakati miamoja wa kiarabu wanatarajiwa kuachiliwa na kurejeshwa makwao, Israel ikilenga kukamilisha shughuli hiyo katika muda wa saa arobaini na nane.

Takriban wanaharakati tisa wa kipalestina walifariki wakati makomandoo wa Irsrael waliposhambulia meli sita zilizokuwa zinaelekea Gaza siku ya jumatatu zikiwa zimebeaba msaada wa chakula na bidhaa zinginezo.

Hata hivyo Israel imetetea hatua ya wanajeshi wake ikisema walikuwa wanajilinda kutokana na uvamizi wa wanaharakati hao, ingawa wanaharakati wenyewe wamekanusha madai hayo.

No comments:

Post a Comment