KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, June 2, 2010

Raia wa Kigeni waachiliwa huru: Israel


Serikali ya Israel, imeanza shughuli ya kuwarejesha nyumbani kikundi cha kwanza cha mamia ya raia wa kigeni waliokamatwa Jumatatu wiki hii, kwenye meli sita zilizokuwa zimebeba bidhaa na chakula cha msaada kuelekea Gaza.

Wanaharakati tisa waliuawa wakati wa operesheni hiyo. Mamia ya wanaharakati wa Kiarabu kutoka Palestina, walipelekwa kwenye mpaka wa Israel na Jordan ambako watu wengi walikuwa wanasubiri kuwalaki.

Israel pia imewaachilia huru raia 200 wa Uturuki ambao wanatarajiwa kurejeshwa nyumbani.

Ripoti zinasema kwamba serikali ya Nchi hiyo, inalenga kuwaachilia huru raia wote wa kigeni waliokuwa wakizuiliwa gerezani katika kipindi cha saa 48 zijazo.

Afisa mmoja mwandamizi katika wizara ya mambo ya nje ya Uturuki, Selin Yemel, amesema uamuzi huo unaonyesha kuwa serikali ya Israel imetambua kosa lake.

Lakini msemaji wa serikali ya Israel amekariri kuwa marufuku dhidi ya meli kuelekea eneo la Gaza bado itaendelea kudumishwa, ili kuzuia silaha kusafirishwa hadi eneo hilo.

No comments:

Post a Comment