KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 12, 2010

Uvutaji sigara wapigwa marufuku Misri

Misri, watumiaji wakubwa wa sigara miongoni mwa nchi za kiarabu, imeanza jaribio la kupiga marufuku uvutaji wa sigara hadharani.

Mji wa Alexandria unatarajiwa kuwa mji wa kwanza Misri kutoruhusu uvutaji wa sigara, ukianza kupiga marufuku kwenye ofisi za serikali.

Wamisri wanavuta takriban sigara bilioni 19 kila mwaka, ambao unazua wasiwasi juu ya afya ya umma.

Misri ni taifa lenye wavutaji wengi wa sigara pamoja na mabomba ya maji ya kiasili yaitwayo shisha yanayopatikana kwenye migahawa, hivyo kuwashawishi Wamisri kuacha itakuwa changamoto kubwa.

Ni jambo la kawaida kuwakuta watu wakivuta sigara kwenye treni, ofisini, na hata hospitalini.

Kwa sasa mjini Alexandria, hayo yanatarajiwa kubadilishwa. Mamlaka ya eneo hilo kwanza yana mpango wa kutia nguvu sheria zilizopo, moja ambayo hudharauliwa, kuzuia uvutaji sigara kwenye ofisi za serikali.

Wamesema katika kipindi cha miaka miwili, sheria ya kuzuia uvutaji sigara mpaka kwenye migahawa utatekelezwa.

Takwimu zinaonyesha Wamisri huvuta takriban sigara bilioni 19 kwa mwaka. Ni tatizo kubwa la afya ya umma
Dr Hassan Salam
Dr Hassan Salam kutoka chuo kikuu cha Alexandria anaongoza utafiti huo.

Amesema, " Kwa bahati mbaya, uvutaji sigara Misri ni jambo la kawaida. Miongoni mwa kila wanaume 10, wanne huvuta sigara na wanawake wengi sasa wanavuta sigara."

Hatua ya kupiga marufuku uvutaji sigara hadharani umeanzishwa kwa mafanikio makubwa duniani kote. Lakini maofisa wanakiri itakuwa changamoto kubwa kuwalazimisha Wamisri kuacha.

Wanatarajia huenda vikwazo vipya angalau vitapunguza idadi ya wavutaji hao na Alexandria iwe mfano kwa nchi nzima.

No comments:

Post a Comment