KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 12, 2010

Hisa za BP zapoteza thamani


Hisa za kampuni ya BP zilipungua thamani kwa asilimia 12, wakati soko la London lilipoanza biashara leo, kwa kuhofia kwamba rais Obama alikuwa aichukulie hatua kali kampuni hiyo.


Hofu ya hatua kali za serikali ya Marekani inadhaniwa imepunguza bei ya hisa za BP
Hisa za kampuni hiyo kubwa zimekaribia kupungua kwa nusu tangu mlipuko uliotokea katika kisima cha mafuta katika ghuba ya Mexico tarehe 20 Aprili.

Bei ya hisa za BP leo zilianzia peni 345, na hii ndio bei ya chini zaidi ya hisa hizo tangu mwaka 1997.

Hata hivyo baadaye bei ilipanda kutoka peni 345 hadi 375.

Uingereza inahofia kwamba kushuka kwa bei hizo za hisa ni jambo ambalo litaiharibia sifa nhini Marekani

Kampuni hiyo imekuwa ikishambuliwa vikali na wanasiasa wa Marekani.

Serikali nayo pia imekuwa ikiitaka kampuni hiyo kutowalipa wenye hisa faida inayopatikana, hadi kazi ya kurekebisha mazingira itakapokamilika, kufuatia kisima chake cha mafuta kuanza kuvuja.

No comments:

Post a Comment