KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, June 12, 2010

Mauaji ya kishirikina yatikisa Kenya


Phillip Onyancha mwenye umri wa miaka 30 amekiri kuwa kwa miaka mitatu iliyopita ameua jumla ya wanawake na watoto 19. Anasema lengo lilikuwa kunywa damu yao.

Mikono yake ikiwa imefungwa kamba, Onyancha amekuwa akiwaelekeza polisi kutoka sehemu moja hadi nyingine ambapo anadai aliiweka miili ya watu aliowaua.

Mwanamume huyo mbaye hadi hivi juzi amekuwa akifanya kazi kama mlinzi anasema yeye ni mshirika wa dhehebu la kishetani ambalo linamhitaji kunywa damu ya watu 100 ili hali yake maishani iwe bora zaidi.

Onyancha anasema alisajiliwa katika dhehebu hilo la kishetani na mwalimu wake wa shule ya upili.

Polisi tayari wameenda katika shule ambapo mwalimu huyo anafundisha hivi sasa lakini hawakumpata.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo iliyopo katika mkoa wa Kati amesema hajui mwalimu huyo wa kike alipo.

Onyancha akishirikiana na wenzake ambao bado hajawataja amekuwa akidai kulipwa fidia kutoka kwa familia za watoto ambao amekuwa akiteka nyara na kuwauwa hata baada ya kulipwa fidia.

Onyancha anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu

No comments:

Post a Comment