KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 12, 2010

Ufaransa yatolewa jasho na Uruguay


Ufaransa na Uruguay zimetoka sare 0-0 kwenye mechi ya pili ya kundi A katika siku ya ufunguzi ya Kombe la Dunia.

Matokeo hayo yana maana kwamba timu zote katika kundi A zina pointi moja kila moja, baada ya wenyeji Afrika Kusini na Mexico kutoka sare 1-1 katika mechi ya ufunguzi.

Uruguay walimaliza mchuano wakiwa wachezaji 10 baada ya Nicholas Lodeiro kupewa kadi nyekundu alipomchezea vibaya mlinzi wa Ufaransa, Bacary Sagna.

Ufaransa walifanya mashambulizi mengi bila mafanikio, na katika kipindi cha pili walifanya mabadiliko, akaingia nahodha wao Thierry Henry badala ya Nicholas Anelka, lakini lango la Uruguay likawa halifunguki.

Mkwaju mkali wa mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Forlan, uliokolewa na kipa wa Ufaransa katika kipindi cha kwanza.

No comments:

Post a Comment