KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, June 10, 2010

Mwanaume Matatani Kwa Kumuiba mtoto


MWANAUME mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Habibu anashikiliwa na polisi mkoani Temeke kwa tuhuma za kumuiba mtoto ambaye awali aliikana mimba yake na kusema mtoto huyo si wake.
Ilidaiwa kuwa mwanaume huyo alifika maeneo ya Tandika mwisho anapoishi mtoto huyo na kuvizia mama wa mtoto huyo hayupo na kisha yeye kuondoka na mtoto huyo kwa lengo ka kumtorosha.

Mtoto aliyetoroshwa na mwanaume huyo ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili na nusu.

Mara baada ya mama wa mtoto huyo kurudi safari aliyokuwa ameenda alikuta mama yake mzazi akihaka huku na huho kumsaka mjukuu wake aliyeachiwa na mwanae huyo wakati ametoka.

Juhudi za haraka haraka za kumsaka kwa majirani wa mtaa mzima pale wanapoishi ziligonga mwamba baada ya mtoto huyo kutoonekana na kuamua kuripoti kituo cha polisi.

Maelezo ya mama wa mtoto aliyatoa kituoni hapo alieleza kuwa alikuwa na mgogoro kati yake na mzazi mwenzake kutaka kupewa mtoto huyo ambaye alimkana mwanzoni na kutompa huduma ya aina yoyote na kuzuka siku za hivi karibuni kutaka mtoto huyo na familia ya mama huyo kupinga matakwa yake.

Hivyo aliiomba polisi kwenda kufanya msako mkali nyumbani kwa mzazi mwenzake huyo na polisi ilipotinga nyumbani kwa HAbibu walimkuta akijiandaa kumsafirisha mtoto huyo kumpeleka mkoani Songea kwa mama yake ili akalelewe huko.

No comments:

Post a Comment