KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, June 12, 2010

Nigeria uso kwa uso na Argentina

Jumamosi Nigeria wanachuana na Argentina katika uwanja wa Ellis Park mjini Johanesburg.

Hii itakuwa mechi ya pili ya kundi la B, itakayotanguliwa na mchuano kati ya timu nyingine za kundi hilo Korea Kusini na Ugiriki.

Kocha wa Argentina, Diego Maradona, amesema anakusudia kuchezesha washambuliaji watatu dhidi ya Nigeria, na anatarajiwa kuwapanga mchezaji bora duniani, Lionel Messi wa Barcelona, Carlos Tevez wa Manchester City na mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Higuai.

Nigeria itawategemea washambuliaji wao wanaocheza Ulaya; nahodha Kanu Nwankwo anayeichezea Portsmouth, Yakubu Ayegbeni wa Everton, Obafemi Martins wa klabu ya Wolfsburg pamoja na Peter Osaze na Chinedu Obasi.

Hii ni mara ya tatu kwa Kanu kushiriki Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment