KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 5, 2010

Simba mmoja amemwuua mfanyakazi wa hifadhi

Simba mmoja amemwuua mfanyakazi wa hifadhi ya wanyama pori yatima nchini Zimbabwe.

Mnyama huyo alitoroka kwenye chumba alichofungiwa kilichoachwa wazi kwa bahati mbaya na kumshambulia Robyn Lotz mwenye umri wa miaka 26.

Taarifa iliyotolewa na hifadhi hiyo ya Chipangali imesema simba huyo mwenye manyoya shingoni, ajulikanayae kama Lobi, alimbwaga chini binti huyo na kushikilia kichwa cha Lotz kwenye mdomo wake.

Mkurugenzi wa hifadhi hiyo alimpiga risasi simba huyo lakini Bi Lotz alikufa kutokana na majeraha muda mfupi baada ya kupelekewa kwenye hospitali mjini Bulawayo.

Shambulio hilo lilitokea siku ya Jumanne asubuhi wakati wafanyakazi walipokuwa wakisafisha malazi ya wanyama hao na kuwatandikia majani.

Mkurugenzi Kevin Wilson alichapisha katika mtandao wa Chipangali, " Kwa hofu kubwa nilimwona Lobi akijikunyata juu ya Robyn, alimwingiza mdomoni mwake huku akiwa amemshikilia kichwani mwake."

Hifadhi hiyo ilianzishwa mwaka 1973 na kuwatunza wanyama yatima, waliotengwa, waliojeruhiwa na waliozaliwa nje ya eneo lao la asili.

No comments:

Post a Comment