KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 5, 2010

Mtetezi wa haki za binadamu auawa DRC

Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Floribert Chebeya amepatikana ameuawa viungani mwa mji mkuu Kinshasa.

Maiti ya Chebeya ilipatikana ikiwa imefunikwa kwa nguo kwenye kiti cha nyuma cha gari lake.

Inaarifiwa bwana Chebeya amewahi kukamatwa na kuteswa na polisi, na kabla ya kuuawa kwake alitarajiwa kufika mblele ya mkuu wa polisi wa Kinshasa mnano Jumanne.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limeelezea kushtushwa na mauaji hayo ya bwana Chebeya ambaye ni mwanaharakati aliyesifika na kuheshimiwa sana nchini Congo.

Kwa mujibu wa shirika hilo, wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini Congo wamekuwa wakiteswa sana baadhi wakitishwa na hata kukamatwa kiholela.

No comments:

Post a Comment