KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 5, 2010

Mwanamke amuuza mwanae Bolivia


Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 30 kutoka makabila ya wazawa ya Bolivia amekamatwa na polisi katika mji wa Cochabamba kwa kumuuza mtoto wake mchanga kwa dola za kimarekani 140.

Duru za polisi kwenye mji wa Cochabamba uliopo katikati mwa nchi hiyo ya Amerika ya kusini zimesema mwanamke huyo amekiri kumwuuza mtoto huyo kwa sababu hana uwezo wa kumtunza.

Jesusa Molle ameiambia polisi kwamba mume wake alimuacha hivyo hana uwezo wa kumudu gharama za matunzo ya mtoto mchanga.

Baadaye Jesusa alikiri kumwuuza mtoto wake wa kike kwa kiasi cha fedha za Bolivia bolivanos elfu moja, sawa na dola za kimarekani 140.

Polisi hao pia wamemnasa mwanamke aliyenunua mtoto huyo, mwenye umri wa miaka 35 aliyesema kuwa aliamua kumnunua mtoto huyo kwa kuwa hakujaliwa kuzaa watoto wake mwenyewe.

No comments:

Post a Comment