Kuanzia sasa shirika la ndege la Oman litaanza safari zake mfululizo kati ya miji ya muscat na Dar-es-salaam.
Safari hizo zitaanza kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Muscat kila siku ya jumamosi, Jumatatu na Jumatano kwa wiki,Ndege Zitakazo geuza kurudi Muscat Zitaanza safari katika kiwanja cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, Dar-es-salaam na kupitia vituo vingine kuelekea Muscat.Shirika la ndege la Oman linafanya safari zake katika vituo 38 Duniani.
Mkurugenzi mtendaji wa Oman Air Way, Peter Hill Anasema: “Oman Air Way imedhamiria kupanua zaidi wigo wake wa kibiashara kwa kuiongeza Dar es Salaam kwenye safari zake na tutafanya kazi hii kwa bidii bila kuchoka ili kuhakikisha tunatimiza malengo yetu.
Mkurugenzi huyo anasema ‘‘ Tukiwa na historia nzuri ya siku nyingi ya kibiashara baina ya Tanzania na Oman tuna uhakika mkubwa sana wa kuendelea kujenga na kuendeleza uhusiano huu wa nchi hizi mbili kupitia huduma zetu za ndege.
Anasema ikijulikana kwa vivutio vyake vya asili, Dar-es-salaam inatazamiwa kuwa na umaarufu wa safari za kitalii zaidi kutoka duniani kote kulingana na thamani yake, Pia kama sehemu maalum ya kufurahia mapumziko ya likizo kubwa za mwaka.
Huduma zetu katika nchi yenye mvuto wa kipekee Tanzania zitaambatana na wasafiri wenye kutambua vitu vizuri na wenye uchaguzi mzuri wa nchi nzuri za kitalii kama Tanzania.
Dar es salaam ndio mji mkubwa zaidi wa kibiashara katika Tanzania ndiyo maana tunaiunganisha Dar es salaam na Dunia.
Anafafanua kwamba ukiwekwa kama mji wa kitalii na njia kuu ya watalii wanaopitia kwenda kupata mapumziko katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Zanzibar tunaamini kwamba tutakua sehemu ya kukuza utalii nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment