KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, June 5, 2010

Mtoto aliyedaiwa kutekwa huyu hapa

MTOTO Grace Kelvin [5] aliyedaiwa kupotea kwa njia ya kutatanisha huyo Hedaru wilayani Same mkoani Same ameonekana maeneo ya Pasua Moshi akiwa amehifadhiwa na wasamaria wema.
Mtoto huyo alipotea majuzi na hakurudi nyumbani kwao hali iliyosababisha wazazi wake waripoti katika vituo vya polisi kwa kupotea kwa mtoto huyo.

Hali ya kupotea kwa mtoto huyo ilileta taharuki hali iliyoababisha wakazi wa maeneo hayo kuhusisha tukio hilo na lile la utekaji watoto na kuwatoa kafara katika msitu na wakazi wa eneo hilo kukerwa.

Katika hali ya wakazi hao kulihusisha moja kwa moja tukio hilo na lille la ut ekaji atoto na kuatoa kafara ilisababisha wakazi hao wa Hedaru kufika kituo cha polisi na kutaka polisi kuwaachia huru watuhumi walioshikilwa kuhusiana na tukio ili kuwaua.

Hata hivyo askari waliokuwa kituoni hapo walizidiwa nguvu na wananchi hao na wananchi hao alijichukulia maamuzi ya kuchoma kituo cha polisi na kuteketea chote kwa moto.

Mtoto huyo alionekana jana maeneo ya Pasua Moshi akiwa amehifadhiwa naw asamaria wema hata hivyo hakikujulikana mara moja alifikaje huko.

Na huyo aliyembeba ni mama yake mzazi Glory Samuel akiwa na furaha tele mara baada ya kumuona mwanae huyo aliyepotea zaidi ya siku tatu.

No comments:

Post a Comment